Monday, 27 June 2016

MPANGO WA BIASHARA




1.0   Utangulizi:
TUNAWEZA WELDERS GROUP(TWG) ni kikundi cha kijamii (CBO) Kimesajiriwa na idara ya maendeleo ya jamii ya Halmashahauri ya Wilaya Muleba kwa Nambari. ZM/KIJ/KU.44./2011  (Hati ya usajiri imeambatanishwa.

1.1   MALENGO MAKUU YA KIKUNDI
        ·            Kuhamasisha ualishaji wa bidhaa kibiashara.
        ·            Kuwajengea uwezo vijana juu ya Elimu ya ufundi  kwa vitendo na ujasiliamali.
        ·            Kuhamasisha vijana wa wilaya ya Muleba kushiriki katika shughuli za maendeleo.
        ·            Kuhamasisha na kuinua vipaji vya vijana
        ·            Kuhamasisha elimu ya ufundi na ujasiriamali.
        ·            Kuafuta vyanzo vya ujenzi na mapao kwa vijana.

1.2   MUUNDO  UONGOI WA KIKUNDI

UONGOZI
UTAWALA (UZALISHAJI)
                                     
MWENYEKITI
KATIBU
MENEJA
 
MWEKA HAZINA
 MHASIBU
KAMATINDOGO NDOGO
AFISA MASOKO
MHUDUMU OFISI

IDARA KIUZALISHAJI
         


1.3  HALI HALISI YA VIJANA KATIKA WILAYA
Wilaya ya Muleba ina idadi ya watu  540,00 kulingana na taarifa ya sensa na makazi ya mwaka 2012.
Vijana kati ya miaka 14 – 35 ni asilimia 30% ya wakazi wote wa  Wilaya;
Nguvu kazi ya Wilaya hutegemea uwepo wa vijana kati ya miaka 14 – 35.
Kuna ongezeko kubwa la vijana wanaomaliza darasa la saba, kidato cha nne na sita na vyuo.
Ni vijana wachache huweza kupata ajira kaika serikali na mashirika.Takribani asilimia zaidi ya 50%  ya vijana hukosa ajira rasmi. Matokeo yanayotokana na ukosefu wa ajira kwa vijana
        ·            Kuongezeka kwa wazururaji
        ·            Uvunjifu wa amani na vitendo vya jinai.
        ·            Umaskini kati ya vijana na jamii
        ·            Magojwa yakuamukiza- Ukimwi na magonjwa ya zinaa
        ·            Madawa ya kulevya.
                             
2.0 HALI HALISI YA  UZALISHAJI.
Mradi mkuu kwa wanachama ni shughuli mbalimbali za ufundi katika karakana ya  SIDA Muleba.
Shughuli hizo ni pamoja na;
        ·            Ukerezaji  vyuma, milango, madirisha n.k
        ·            Ujenzi
        ·            Utengenezaji magari na pikipiki
        ·            Ufundi seremela
        ·            Ufundi umeme

Wateja wa uzalishaji huu upatikana ndani na nje yaWilaya ya Muleba; Ikwemo.
        ·            Watu binafsi
        ·            Makampuni
        ·            Mashirika
        ·            Serikali
        ·            Hali halisi ya kiuzalishaji ni asilimia 20% ikitokana na ukosefu wa nyenzo za kufanyia kazi.
        ·            Pato la mwanachama wa kawaida huwa ni chini ya Dola  1  ya kimarekani hii hupelekea mafundi wengi kufanya kazi kwa ajiri ya kupata fedha ya kujikimu tu (Subsistence income)




3.0 MATARAJIO KIUZALISHAJI

Aina ya ufundi
Mwaka 1
Mwaka  2
Mwala  3
Jumla
Ukerezaji
16,000,000/=
19,500,000/=
67,000,000/=
102,000,000/=
Ufundi pikipiki/ magari
14,600,000/=
16,000,000/=
19,700,000/=
50,300,000/=
Ufundi umeme
16,000,000/=
17,900,000/=
19,000,000/=
52,900,000/=
 na mabango
4,000,000
6,000,000/=
9,000,000/=
19,000,000/=
                                   JUMLA   TSH.                                         222,100,000/=


MKAKATI  WA MASOKO.
-         Kutakuwa na mkakati wa masoko ili kuongeza kiwango cha wateja na mauzo.
v Mikakati hiyo itakua kama ifuatavyo;
·        Kufunga mikataba na mawakala
·        Kutengenea alama  za biashara (Trade mark),  pamoja na nembo ya biashara; (Business Logo)
·        Kutengeneza Tovuti ya biashara ya kikundi
·        Kusimamia na kuongeza ubora wa biashara (Quality Control)
·        Kutengeneza vipeperushi (Brochures)
·        Kufanya matangazo ya wazi
·        Kufanya matangazo kupitia vyombo vya habari (Magazeti na Redio)
·        Kuhudhuria maonyesho ya nane nane











MPANGO WA  BIASHARA   WA    KIKUNDI
CHA
TUNAWEZA WELDERS GROUP(TWG)



MUDA: 2016 – 2018



ANWANI :P:O:BOX 205 Muleba
BARUA PEPE:tunaweza-muleba
SIMU: 0763667592

No comments:

Post a Comment